“HII
sasa ni kufuru!” Hivi ndivyo utakavyoweza kusema kwa Davies Mosha
ambaye ni makamu mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, ambaye nafasi
yake kwa sasa klabuni hapo inashikiliwa na Clement Sanga.
Kwa
tafsiri ya haraka, yawezekana Mosha anaweza kuwa ndiye kiongozi pekee
wa soka nchini kumiliki gari la kifahari na lenye gharama kubwa aina ya
Lamborghini kama ambalo linamilikiwa na mshambuliaji wa
Manchester United, Wayne Rooney.
Manchester United, Wayne Rooney.
Gari
analomiliki Mosha ambalo lina rangi ya njano, linaaminika kuwa miongoni
mwa magari yenye thamani kubwa siyo tu Tanzania na Afrika, bali duniani
kote, kwani hata siku Rooney alipolinunua wenzake wengi hawakutegemea,
siyo kwa sababu hana fedha, ila kwa kuwa hakuwa mtu wa matumizi ya
magari yenye thamani kubwa kama hilo.
Mosha ameliambia Championi Ijumaa kuwa anamiliki magari kadhaa ya kifahari kwa matumizi yake binafsi na familia yake.
Yafuatayo
ni maelezo kuhusiana na gari hilo la kifahari kwa kuanzia kiwango cha
mafuta na usumbufu anaoupata akiwa katika mizunguko yake.
Ameinunua kwa bei gani?
“Kutokana
na ubora wa gari hili, nililazimika kutoa shilingi bilioni moja kwa
ajili ya kulinunua, kama unavyojua ni fedha nyingi, nimenunua kwa
mapenzi yangu.
Alipolinunua
“Hili gari kaniuzia mtoto wa Bakhresa (Yusuph), baada ya kufikia makubaliano kati yake na mimi, aliniuzia Julai 2011.
Spidi ya gari
“Hili gari kasi yake ya mwisho ni 360, ni kasi kali na inatosha kwa matumizi yangu binafsi.
Matumizi ya mafuta
“Matumizi ni ya kawaida wala siyo ya kuogopesha sana, inategemea na umbali utakaotembea.
Usumbufu anaoupata
“Usumbufu
mkubwa ninaoupata kiukweli, nikiwa naendesha barabarani, madereva
wengine wanalishangaa sana, hali inayosababisha kutokea ajali au
msuguano mara kadhaa.
“Hivi
karibuni dereva mmoja aliigonga sehemu ya tairi la nyuma kushoto
kutokana na kuishangaa, ilikuwa maeneo ya Masaki hapahapa Dar es Salaam.
“Matengenezo
yake yaligharimu pauni 20,000 (zaidi ya shilingi milioni 50), hali
iliyosababisha niwe makini nikiwa naendesha,” anasema Mosha.
“Matengenezo
yake yaligharimu pauni 20,000 (zaidi ya shilingi milioni 50), hali
iliyosababisha niwe makini nikiwa naendesha,” anasema Mosha.
No comments:
Post a Comment