BONDIA
Francis Cheka, ameapa kwamba hatopanda ulingoni tena kucheza na
mabondia wa Tanzania huku akidai pambano lake na Karama Nyilawila la
Septemba 29, mwaka huu ndiyo litakuwa la mwisho.
Mabondia hao watapanda ulingoni kuwania ubingwa wa UBO katika pambano la uzito wa kg. 75 raundi 12.
Pambano hilo litasimamiwa na Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST) litakalofanyika katika Ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
Katika pambano hilo kutakuwa na mapambano utangulizi 12 kutoka kwa mabondia chipukizi.
Akizungumza
kwa simu jana, Cheka alisema pambano lake na Nyilawila anaamini
litakuwa ni kubwa na lenye msisimko kwani wote wote na uwezo mkubwa na
wanarekodi nzuri katika michezo ya kimataifa.
Alisema
kutokana na uzito wa pambano hilo ndiyo maana aliamua kusaini mkataba
na promota moja kwa moja, ingawa alikuwa ameshakataa kupigana hapa
nchini kwa kuwa mobondia wote hawana hadhi na viwango vyao kuwa chini
hivyo kuhofia kuvuruga rekodi yake.
"Nitapigana
na Nyilawila na nipo tayari kwani natambua uwezo wake ni mkubwa, licha
ya kuwa nilishawahi kumpiga kwa pointi katika pambano letu tulilocheza
Morogoro lakini nasema hili la sasa ndiyo litakuwa la mwisho kucheza na
mabondia wa hapa nchini," alisema.
Aliongeza
kuwa kwa sasa anaendelea kujifua kwa ajili ya pambano hilo, kwani
anajua anamuda mrefu wa kujiandaa na anaahidi kuchukua ubingwa huo.
No comments:
Post a Comment