18 December 2011

Kafulila afukuzwa NCCR – Mageuzi




AMPIGIA MAGOTI MBATIA KWA MACHOZI, WAJUMBE WAKATAA KUMSAMEHE
Na Fidelis Butahe
CHAMA  cha NCCR- Mageuzi kimemfukuza uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini,  David kafulia na wajumbe wengine sita akiwamo aliyekuwa mgombea urasi wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, Hashim Rungwe.Uamuzi huo ulitolewa kwenye kikao cha dharura  cha Halmashauri Kuu Nec ya chama hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa  Poroin jijini Dar es Salaam jana, ambao ulitawaliwa na vurugu mpaka polisi wakaitwa ili kuongeza ulinzi.
Baada ya uamuzi huo kutolewa Kafulila alikwenda kupiga magoti mbele ya Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia huku akibubujikwa machozi na kuomba radhi akisema: “Naomba radhi, nimekosa mnisamehe...”

Baada ya hapo Mbatia alisimama na kumwombea msamaha  kwa wajumbe wa kikao hicho, lakini walikataa na kumweleza (Mbatia) kuwa akisamehewa watarudisha kadi zao za uanachama.“Hatutaki , Kafulila hatufai anakiharibu chama na akisamehewa  sisi tutarudisha kadi zetu za uanachama ili ubaki naye kwenye chama...,” walisikia wajumbe  hao wakisema kwa sauti ya juu.Wanachama wengine waliofukuzwa ni, Ally  omari, Mbwana Hassan, Josam Rugugila, Lucy Kapya, Jamwe Batifa na Hashim Rungwe ambao walikuwa viongozi wa chama hicho. 

chanzo mwananchi

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname