14 February 2016

Kauli ya Diamond Platnumz yamfanya Mrisho Mpoto asitishe kuachilia video ya 'Sizonje

Kauli ya staa wa muziki Diamond Platnumz ‘Kuna kushoot video na kurekodiwa’ imemfanya msanii wa muziki wa asili Mrisho Mpoto kuitia kapuni kwanza video yake mpya ya wimbo ‘Sizonje’ ili aichunguze kwanza kama inafaa.

Kupitia ukurasa wa instagram, Mpoto ameandika "Diamondplatnumz post yako ya leo imenifanya nisile Siku nzima. Nikiitafakari na sasa nimeamua kusitisha kutoa video yangu mpya ya #SIZONJE maana sina uhakika kama nime shoot au nimerecord. Ukimkimbiza sana mjusi anageuka kuwa nyoka"

Ijumaa hii Diamond aliachia video mpya ya wimbo ‘Make Me Sing’ akiwa na AKA wa Africa kusini na kutwitter.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname