09 February 2016

Jux azungumzia kuwasiliana na Jackie Cliff na hali yake kwa sasa akiwa gerezani nchini CHINA

jackjack4
Msanii wa rnb Jux amesema Jackie Cliff aliyedaiwa kukamatwa na madawa ya kulevya nchini China na kufungwa jela, yupo salama na amekuwa akiwasiliana nae mara kwa mara.
Akizungumza na Clouds FM Jumatatu hii, Jux alisema anashindwa kuzungumzia vitu vingine vya ndani kwa kuwa mwanadada huyo hapendi.
Jux alisema “Huwa tunafanya mawasiliano ingawa sio mara kwa mara. She is okay, yuko sawa. Nimewasiliana naye kama miezi miwili iliyopita. Siwezi kuongelea sana vitu vingine hata hivyo yeye mwenyewe hapendi niwe naongea ongea na watu kuhusu maisha yake, Kuna ndugu zake wanasikia, kuna watu wa karibu, pia kuna watu wengine wanaposikia sikia, wanaweza kuona kama mimi nachukua advantage yake, kwa sababu kila mtu ana niuliza vipi fulani vipi fulani, ndio maana muda mwingine anasema acha usiongee ongee,”
Jux aliwahi kuripotiwa kuwa na mahusiano na Jacky

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname