Mugeta (wa kwanza kushoto)
Kijana wa Kitanzania Emily
Mugeta ametambulishwa katika timu yake mpya ya Neckarsulm Union Sports
yenye makazi yake mjini, Neckarsulm nchini Ujerumani.
Timu hiyo inacheza ligi ya
Verbandsliga ambayo ni miongoni mwa ligi za Ujerumani ambazo zina majina
tofauti kama vile Bundesliga, second Bundesliga, Third Bundesliga.
Ili kuingia Verbandsliga unatakiwa kupitia kwanza Oberliga.
Wakwanza kushoto ni kocha wa timu hiyo, Torsten Damm anayemfuatia ni Mugeta
Mugeta amepigwa picha hizi juzi
walipoanza mazoezi ambapo wanajiandaa na mechi ya kutambulishwa rasmi
kwa timu nzima ambayo watachuana na Hoffeinheim Julai 15 mwaka huu.
Kila la kheri Mugeta katika maisha yako ya soka huko Ujerumani, bila shaka utaiwakilisha vyema Tanzania.
No comments:
Post a Comment