01 July 2015

MTOTO ALIYEZALIWA JELA AREJEA NA KUMTOA MAMA YAKE GEREZANI

Kanhaiya Kumari (kushoto) akiwa na mama yake, Vijaya mara baada ya kuachiwa huyu.
Mtoto mdogo wa kiume wa mwanamke ambaye amedhoofika kwenye jela kwa takribani miaka 20 nchini India kwa upungufu wa Pauni za Uingereza 119 katika pesa za dhamana hatimaye amehakikisha kuachiliwa huru kwa mama yake.

Kanhaiya Kumari, mwenye umri wa miaka 19, alizaliwa ndani ya gereza na Vijaya, mwenye miaka 48, ambaye alikamatwa mwaka 1993 kwa kuhusiana na kesi inayohusisha mauaji ya mmoja wa majirani zake katika wilaya ya Aligarh nchini India.
Alipatiwa dhamana mwaka 1994 lakini - ilitupwa na mumewe - hakuwa na uwezo wa kulipa Rupia 10,000 iliyokuwa ikihitajika kuhakikisha uhuru wake. Sasa ameungana tena na mtoto wake wa kiume, baada ya mtoto huyo kuwa amefanya kazi kupata pesa hizo za dhamana na kuishawishi Mahakama Kuu kwa ajili ya kuachiliwa mama yake.
Kanhaiya alikana kuhusika kwa namna yoyote katika kesi hiyo ya kihistoria ya mauaji kwenye kijiji cha Mahrauni mjini Aligarh.

Alikamatwa huku akiwa na ujauzito wa miezi mitano, akajifungua mtoto Kanhaiya huku akiwa amefungwa jela, ambapo baadaye mama na mtoto walipelekwa katika gereza la Nari Niketan lililoko Lucknow, Uttar Pradesh.
Vijaya alipewa dhamana na mahakama mwaka 1994, lakini mumewe aligoma kutuma pesa za dhamana kiasi cha Rupia 10,000.
Kanhaiya alipelekwa kwenye jela ya watoto mjini Lucknow akiwa na umri wa miaka 11, ambapo alitumikia miaka 7 kabla ya kuachiwa huru mwaka jana.
Mapema tangu kuruhusiwa kutoka kwenye jela hiyo, Kanhaiya akapata kazi katika kiwanda kimoja na kujipanga kukusanya kiasi cha pesa za dhamana ili kumwezesha mama yake kuachiwa huru.
Aliishawishi Mahakama Kuu ya Allahabad kumwachia Vijaya, na hatimaye akapatiwa dhamana na kuungana tena na kijana wake nje ya kuta za gereza hilo Mei 5.
"Habari ya Vijaya inashangaza. Mtoto wake wa kiume, alizaliwa jela, mwishowe akamtoa humo," alisema mkuu wa gereza la Nari Niketan, Shashi Srivastava.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname