05 July 2015

KINACHOFUATA TOKA KWA ALIKIBA KIMATAIFA MWAKA HUU!

Alikiba ambaye ameachia video ya‘Chekecha Cheketua’ wiki hii, janaalipata nafasi ya kuchati na mashabiki
wake kupitia ukurasa wa Facebook wa Coca-Cola. Muimbaji wa ‘Chekecha
Cheketua’, Alikiba ambaye yuko Nairobi, Kenya kwenye msimu mpya wa kipindi cha Coke Studio Africa,
ametoa ahadi kwa mashabiki wake juu ya collabo ya kimataifa. Miongoni mwa maswali aliyokutana
nayo ni kuhusiana na collabo ya kimataifa, ambapo shabiki mmoja alimpongeza kwa kazi zake na kumuuliza ni lini waitegemee, na hili ndio jibu lake: “Ahsante sana. Mwaka huu huu.” Hata hivyo King Kiba hakutoa maelezozaidi, hivyo collabo hiyo bado iko kwenye mabano. Unahisi ni msanii gani wa kimataifa ambaye Kiba anafaakufanya naye collabo kwa kipindi
hiki?

 


BOFYA HAPA KUONA VIDEO  KIBA AKIFUNGUKA KUHUSU COLLABO HIYO 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname