08 July 2015

KAMPUNI YA LG YATOA ZAWADI MBALIMBALI KWA WATEJA WAKE WAKATI WA SIKUKUU YA SABASABA

Mkufunzi mwandamizi toka kampuni ya LG, Elizabeth Morris, (Kulia) akimpa mkono na Bw. Festo Sakaya (kushoto) baada ya mteja huyo kujinunulia friji la kisasa ndani ya banda lao la maonyesho ya Sabasaba ambapo baada ya kufanya manunuzi alizawadiwa microwave ya bure, ya LG. Kampuni hiyo ipo kwenye promosheni ya punguzo la bidhaa zake kwa asilimia 15 kwa msimu huu wa sabasaba na ramadhani. Katikati ni meneja wa tawi la LG Mtaa wa Nkurumah Bw. Yasin Lodhi

Mkufunzi mwandamizi toka kampuni ya LG, Elizabeth Morris, (Kushoto) akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya microwave ambayo inatolewa kama zawadi kwa wateja wanaonunua friji za kisasa za LG. Tukio hilo lilifanyika katika banda la LG ndani ya viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara kimataifa maarufu kama Sabasaba, wa pili kushoto ni meneja wa tawi la LG Mtaa wa Nkurumah ,Yasin Lodhi

Bw. Festo Sakaya akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupokea zawadi ya Microwave ya kisasa toka LG ambayo aliipata baada ya kufanya manunuzi ya friji la kisasa ndani ya banda la LG wakati wa maonyesho ya 39 ya biashara kimataifa maarufu kama Sabasaba

Meneja wa tawi la LG Mtaa wa Nkurumah, Yasin Lodhi, (kulia) akikabidhi zawadi ya Microwave kwa Bi. Hidaya Kapera, (kushoto) mara baada ya mteja huyo kufanya manunuzi ya bidhaa za kisasa ndani ya banda la LG katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara maarufu kama Sabasaba. 


 Hidaya Kapera, akiondoka na zawadi yake ya Microwave baada ya kufanya manunuzi ya bidhaa za kisasa ndani ya banda la LG katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara maarufu kama Sabasaba

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname