06 July 2015

DIAMOND AFANYIWA KUFURU NIGERIA

Staa grade one kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Pasua anga! Staa grade one kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefanyiwa kufuru ya bonge la pati na msanii mwenzake kutoka nchini Nigeria, Kingsley Chinweike Okonkwo ‘KCEE’ Ijumaa Wikienda lina ubuyu kamili.Kwa mujibu wa chanzo cha karibu kilichosafiri na staa huyo ambaye yupo nchini humo kwa ziara yake inayofahamika kama ‘Nana Tour’, tangu Diamond alipofika siku ya kwanza akiwa na mameneja wake, Salam, Babu Tale, DJ wake aitwaye Romy Jones na wengine, mastaa kibao wakubwa walikuwa wakihitaji kuwa wenyeji wake.
“Jamaa ana uhusiano mzuri sana na mastaa wa Nigeria. Kuna ambao ameshafanya nao kazi kama Yemi Alade, Tiwa Savage, Bracket, Iyanya, KCEE na P Square (bado haijatoka). “Pia wapo wengine kibao wanaotaka kufanya naye kazi hivyo wanamuwinda.
Waliposikia anakuja kufanya ziara ya wimbo wake mpya kila mmoja alitaka kuwa mwenyeji wake. 


No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname