07 July 2015

Balotelli afiwa na Baba yake, achelewa kufika mazoezini



Kwa mujibu wa gazeti la The Telegraph, mchejazji wa klabu ya Liverpool na timu ya Taifa ya Italia Mario Balotelli jana amemiss mazoezi ya kwanza ndani ya klabu yake baada ya kupata msiba wa Baba yake aliyewahi kumlea kipindi ana miaka mitatu.
Msiba huo uliotokea mwisho mwa wiki iliyopita umemfanya Balotelli achelewe kufika mazoezini, ambapo sasa ameongezewa likizo lakini uongozi wa klabu ya Liverpool unaamini mchezaji huo atawahi kujiunga na wenzake siku yoyote kabla ya mwisho mwa wiki ijayo ambapo Liverpool itasafiri Mashariki ya mbali na Australia kwa ajili ya mechi za kujipima nguvu.
Baba huyo mlezi alikuwa anaitwa Francesco na amefariki huko nchini Italia

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname