Azam FC inashusha wachezaji
sita mahiri kwa majaribio ya kujiunga na kuimarisha kikosi cha msimu
ujao ambacho pia kitawakilisha nchi kwenye mashindano ya CECAFA Kagame
Cup wiki tatu zijazo na Kombe la shirikisho hapo mwakani.
Wachezaji wanaokuja kwa
mazungumzo, majaribio na kupima afya zao kabla ya kujiunga na kikosi cha
Stewart Hall ni pamoja na mshambulizi anayeongoza kufumania nyavu
kwenye ligi ya Zambia toka klabu ya Nkana Red Devils Jimmy Ndhlovu
ambaye awali alikuwa akicheza kwa mkopo kwenye klabu ya Power Dynamos.
Jimmy tayari amekuwa kwenye rada za vilabu vingi vya Afrika Kusini hasa
Morroka Swallows ambao wanamnyatia hivi sasa.
Tovuti ya Azam FC imesema
kwamba, katika orodha hiyo yumo mshambulizi toka nchini Uingereza Joe
Dickson ambaye kocha Stewart Hall anamfahamu vema kama ilivyo kwa kiungo
mchezeshaji Ryan Burge kutoka nchini Uingereza pia.
Jean Baptiste Mugiraneza (Migi )
ni kiungo mwenye uwezo wa kucheza kwa ufasaha nafasi ya ulinzi kama
ilivyokuwa kwa Mutesa Patrick Mafisango. Kwa sasa Migi anakipiga kwenye
klabu bingwa nchini Rwanda ya APR na timu ya taifa ya Rwanda Amavubi.
Habari za ujio wa Migi zilikwisha vuja kwenye baadhi ya vyombo vya
habari nchini Rwanda, Uganda na Tanzania na sasa klabu ya Azam FC
inathibitisha kuwa mchezaji huyu wa zamani wa Kiyovu Sports FC mwenye
uzoefu mkubwa na mikikimikiki ya soka la Afrika Mashariki atatua nchini
baada ya kumaliza majukumu yake na timu ya Taifa ya Rwanda.
Kama hao hawatoshi Azam FC pia
inawaleta magolikipa wawili wenye uwezo mkubwa na uzoefu wa kutosha na
mikikimikiki ya soka la Afrika ili kwenda sambamba na vilabu
vinavyotamba barani Afrika, wachezaji hao ni Vincent Atchouailou De Paul
Angban kutoka klabu ya Juanesse ya kwao Ivory Coast na mlinda lango
Mcameroon Nelson Bongaman toka DCMP ya Kishasa DRC
No comments:
Post a Comment