Klabu
ya ‘Wekundu wa Mimbazi’ Simba imesema inatarajia kumsanisha mkataba
mshambuliaji wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Uganda Hamisi Kiiza
‘Diego’ ili kuiongezea nguvu safu yao ya ushambuliaji kwa ajili ya msimu
ujao.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili
ya Simba Zacharia Hans Poppe amesema, kuna mtu alikuwa nashughulikia
suala hilo na kila kitu kimekwenda vizuri kilichobaki ni makubaliano ya
mshahara wa mkali huyo na mambo mengine madogomadogo ili aweze kumwaga
wino kujiunga na vijana wa Msimbazi.
“Kuna mtu alikuwa anashughulikia
hilo suala lakini nafikiri yamebaki mambo madogo sana, tumeamua
kumchukua Kiiza ili aongeze nguvu pale kwenye ‘striking force’”, amesema
Poppe.
“Kama walishafikia makubaliano
basi kilichobaki ni kusaini mkataba, makubaliano kwamba ni kiasi gani
cha mshahara atalipwa, mambo ya marupurupu na vitu kama hivyo
tukikubaliana hapo atasaini mkataba”, ameeleza.
“Kunawachezaji wengine wawili
mmoja midfielder mwingine striker nafikiri kufikia kesho au keshokutwa
tutawapa habari zake kamimili”, alimaliza.
Klabu ya ‘Wekundu wa Mimbazi’
Simba imesema inatarajia kumsanisha mkataba mshambuliaji wa zamani wa
Yanga na timu ya taifa ya Uganda Hamisi Kiiza ‘Diego’ ili kuiongezea
nguvu safu yao ya ushambuliaji kwa ajili ya msimu ujao.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili
ya Simba Zacharia Hans Poppe amesema, kuna mtu alikuwa nashughulikia
suala hilo na kila kitu kimekwenda vizuri kilichobaki ni makubaliano ya
mshahara wa mkali huyo na mambo mengine madogomadogo ili aweze kumwaga
wino kujiunga na vijana wa Msimbazi.
“Kuna mtu alikuwa anashughulikia
hilo suala lakini nafikiri yamebaki mambo madogo sana, tumeamua
kumchukua Kiiza ili aongeze nguvu pale kwenye ‘striking force’”, amesema
Poppe.
“Kama walishafikia makubaliano
basi kilichobaki ni kusaini mkataba, makubaliano kwamba ni kiasi gani
cha mshahara atalipwa, mambo ya marupurupu na vitu kama hivyo
tukikubaliana hapo atasaini mkataba”, ameeleza.
“Kunawachezaji wengine wawili
mmoja midfielder mwingine striker nafikiri kufikia kesho au keshokutwa
tutawapa habari zake kamimili”, alimaliza.
No comments:
Post a Comment