Miezi ya hivi karibuni Nay Wa Mitego aliamua kumchukua mtoto wake kutoka kwa mama yake Siwema aliyekuwa akiishi jijini Mwanza baada ya kutoelewana kati yao na minong’ono ilisambaa kuwa msanii huyo anatoka kimapenzi na Shamsa Ford.
Hata hivyo wote wawili walikana kutoka kimapenzi na kwamba ni marafiki wa kawaida,Clouds Fm imezungumza na Nay kuhusu picha hiyo alisema kuwa mwigizaji huyo ni rafiki wa dada yake alienda kumtembelea na kumbeba mtoto huyo na kupiga naye picha.
‘’Siyo kweli kwamba mtoto wangu analelewa na Shamsa namlea mwenyewe na mama yangu alienda kumtembelea dada yangu akapiga picha na Curtis,’alisema Nay.
No comments:
Post a Comment