Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji
amesema atajiuzulu wadhifa wa uenyekiti iwapo itabainika kuwa kweli yeye
ni fisadi, mwizi na muongo kama ambavyo Mwenyekiti Mtendaji wa
Makampuni ya IPP, Reginald Mengi amekuwa akisukuma mashambulizi dhidi
yake.
Manji amezungumza na waandishi wa
habari kwenye makao makuu ya Yanga, leo na kueleza hayo huku
akisisitiza kumtaka Mengi ajitokeze na wakutane kwa ajili ya kufanya
mdahalo wa wazi ambao utadhibitisha kuhusiana na tuhuma hizo.
Alisema kuendelea kuiongoza Yanga
wakati imethibitika ni fisadi na mwizi, ni utovu wa nidhamu na
wanachama wa klabu hiyo watamtilia shaka.
Bilionea huyo ameyasema hayo leo
Jumapili, mbele ya wanachama wa klabu hiyo kwenye mkutano uliofanyika
Makao Makuu ya Yanga, makutano ya Mitaa ya Jangwani na Twiga jijini Dar.
Manji alifunguka kuwa Mengi amekuwa akimsakama kwa muda mrefu na sasa amesema amechoka.
Manji anadai kilichomchefua zaidi
ni habari iliyotoka kwenye Gazeti la Nipashe kuwa kampuni yake ya Farm
Equip Tanzania and Quality Garage, ijulikanayo kama QG Engineering
ilishindwa kulipa kiasi cha bilioni 9.055 serikalini.
Manji amekanusha taarifa hiyo na
kuomba Julai 3, mwaka huu kukutana na mmiliki wa gazeti hilo, Mengi
kwenye mdahalo ‘live’ na kila upande uje na ushahidi wa kutosha kisha
Watanzania wapige kura ili muongo na mkweli ajulikane kuliko kuchafuliwa
jina.
“Iwapo itabainika kweli mimi ni
fisadi, muongo na mwizi, niko tayari kuachi ngazi ya uenyekiti wa Yanga
na sitagombea cheo chochote hapa, maana klabu itakuwa inaongozwa na mtu
asiye na vigezo sitahiki vya kuwa kiongozi,” alisema Manji.
“Watu wanapaswa kujiuliza, mimi
ni fisadi ninayejulikana na vyombo vya habari vya IPP tu? Wengine
hawaoni hilo? Je, kwa nini IPP pekee ndiyo waone mimi ni fisadi? hapo
watu wajiulize,” alisema Manji.
Source: Salehjembe
No comments:
Post a Comment