25 May 2015

Huu ndio mshahara mpya wa Said Ndemla baada ya leo kusaini mkataba wa miaka mitatu Simba

ndemla
Ndemla (kulia) akisaini mbele ya Rais wa Simba, Evans Aveva (kushoto)
WEKUNDU wa Msimbazi, Simba wameanza harakati za kuwabakisha nyota wake waliomaliza mikataba baada ya jioni ya leo kumsainisha mkataba wa miaka mitatu (3) kiungo wake mchezeshaji, Said Ndemla.
Ndemla amesaini mkataba huo mbele ya Rais wa Simba, Evans Aveva wenye thamani ya shilingi milioni 40 za Kitanzania jumlisha gari aina ya IST.
Nyota huyo zao la Simba B atakuwa analipwa mshahara wa milioni mbili (2) kwa mwezi.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname