06 February 2015

Madaktari wamuomba Bobby Brown awaruhusu wazime mashine inayomsaidia Bobbi Kristina kupumua sababu hakuna matumaini

Madaktari wa hospitali alipolazwa aliyekuwa mtoto wa mwanamuziki wa nchini Marekani,marehemu Whitney Houston, Bobbi Kristina hawana tena matumaini ya kuokoa maisha ya binti huyo.
Madaktari hao wamemuomba baba yake Bobby Brown kutoa ruhusa ya kuzima mashine inayomsaidia kupumua ikiwa na maana kwamba kukubali matokeo ya kuwa hawezi kupona,TMZ imeripoti.

Vyanzo vya familia hiyo vimeiambia TMZ kuwa maamuzi sasa yako mikononi mwa baba yake Brown, na inadaiwa kuwa hataki kufanya maamuzi hayo magumu hivi sasa anasubiri mpaka baada ya weekend.


Vyanzo hivyo vimeongeza kuwa Brown bado ana matumaini kuwa binti yake anaweza kupona sababu kuna mtu wa familia yake aliwahi kutoka kwenye coma baada ya siku nane.

1 comment:

Comments system

Disqus Shortname