12 February 2015

Hii ndiyo siri aliyoitoa Vanessa Mdee kama msanii ukitaka kuwa balozi wa brand kubwa, fanya hivi

Vanessa Mdee ni balozi wa makampuni makubwa mawili nchini Tanzania.

Akiongea nasi hivi karibuni, Vanessa alidai kuwa inahitaji qualities kadhaa kwa msanii kuweza kupewa kazi hiyo.

Kikubwa sana ni msanii ni kujithamini na kujitambua kama a brand yeye mwenyewe kama msanii au mtu ambaye unafanya sanaa. Uwe muigizaji, muimbaji yeyote yule,” alisema Vanessa.

Bidhaa zipo nyingi sana duniani. Naamini kuwa kila msanii ambaye atajirepresent kama brand atapata bidhaa ambayo ingependa kuambata naye kwasababu wamefanana. Kwahiyo tafuta kitu ambacho ni special kwako. Ni vitu vya kuzingatia kujitambua na kujifahamu kama brand na kitu gani unachokiweza zaidi.”

Naamini kwa kufanya hivyo itawafungulia wasanii wengi milango mingine ya kufanya endorsement ni muhimu sana kwa msanii,” alisisitiza.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname