03 January 2015

HIVI NDO PANYA ROAD WALIVYO TIKISA JIJI LA DAR JANA JIONI


Chanzo cha panya road kuvamia jiji nzima leo ni kwamba kuna mwanachama mwenzao aliuawa na sungusungu majuzi walipokwenda kuiba.kwa hiyo jana walipitisha michango na leo mida ya saa kumi jioni walikusanyika magomeni kagera.karibu na friends corner hotel kwa ajili ya mazishi.kwa macho yangu nilishuhudia ni kundi kubwa kama la vijana miatano wanasubiri kwenda kuzika kumbe wote hao ni panya road fikiria.kumbe kuanzia jana wamepeana taarifa jiji nzima waje wakimaliza kuzika waanze kulipa kisasi jiji nzima.ilipofika muda wa kwenda kuzika walifunga barabara na kuanza kuwapora makonda na kuelekea makaburini ktk makaburi ya kagera mikoroshini,kipindi hicho polisi walipata taarifa na wakidhani wanaenda kuzika ktk makaburini ya mburahati wakawa wanawasubiri kule kumbe sivyo.makaburini maiti ilizikwa kwa amri uku mashee wakishurutishwa na mapanga.walipotoka kuzika ikawa balaha wakarudi morogoro road nakuanza uporaji hadi polisi walipofika na kupiga mabomu, na kuanza kuwakimbiza na kufanikiwa kuwakamata wawili.lile kundi baada ya kutawanyika basi wale wanaoenda mbaghala njia nzima wanapora,wa buguruni tabata na gongolamboto nao walikuwa napora na na kundi la mwananyama ndilo lilirudi tena usiku huu na kufukuzana na polisi hadi mida hii morogoro road nyeupe hata bodaboda ni shida kuipata.uzembe mkubwa ni polisi hawakujipanga kwani walijua kila kitu nau vijana waliwaona sasa sijajua intelejisia yao imekaa vipi kukabili hawa vijana wadogo ukiwatazama umri ni miaka 14-23

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname