05 December 2014

MADHARA YA POMBE ZA OFA! ALEWA AZIMIA WAHUNI WAMUUZA!

Kijana akiwa katika hali ya kutojitambua baada ya kupata ulabu wa Kutosha. Kwa mujibu wa chanzo makini, jamaa huyo alikuwa na mwenzie ambaye inadaiwa kuwa ni kabila moja kwenye gari ambapo aliposimama maeneo hayo aliwaambia watu kuwa mwenzake huyo alikuwa amelewa baada ya kufakamia pombe za ofa. 

HII kali! Jamaa mmoja ambaye jina lake halikutambulika mara moja, alikutwa amelazwa chini akiwa amelewa chapachapa, maeneo ya Mtaa wa Kongo, Kariakoo jijini Dar, huku kawekewa karatasi kifuani na wahuni ikisomeka; “for sale” (anauzwa). 
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, mwenzake huyo baada ya kuona swaiba wake hajitambui, aliamua kumshusha maeneo hayo na kumlaza chini kisha kumuwekea karatasi kifuani iliyokuwa na maandishi yaliyosomeka; “for sale”.Chanzo kiliendelea kuweka wazi kuwa mtu huyo alianza kuwaambia watu waliokuwa wamekusanyika mahali hapo kuwa kama kuna mtu ana shida na ‘mtoto’ anapatikana kwa bei ya maelewano huku akiwakataza kumpepea. 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname