05 December 2014

MADAI MAZITO: AUNT EZEKIEL ANASA MIMBA NJE YA NDOA

Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel akiwa viwanja na shosti yake, Wema Sepetu.

Madai mazito! Pamoja na kutumia nguvu kubwa kukanusha kwa miezi kadhaa, bado staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson, anaendelea kugandwa na madai kwamba, amenasa mimba nje ya ndoa, Ijumaa lina mkanda kamili.

Habari hizo zilishika kasi mithili ya moto wa kifuu baada ya Aunt kunaswa Klabu ya New Maisha iliyopo Masaki jijini Dar, Jumapili iliyopita akiwa ameshiba yaani kitumbo ndi huku akishindwa kukificha baada ya kila kitu kuonekana waziwazi kwa macho yasiyohitaki miwani.

KIGAUNI CHAANIKA KILA KITU
Aunt, akiwa ukumbini humo na mastaa wenzake waliohudhuria kwenye shoo ya msanii wa Bongo Fleva aitwaye Mirrow anayesimamiwa na kampuni ya muigizaji, Wema Isaac Sepetu na Meneja Petit Man, alitinga akiwa amevaa kigauni cha drafti nyeupe na nyeusi ambacho kilionesha vilivyo tumbo lake.
WEMA ADAIWA KUMSINDIKIZA KLINIKI
Kwa mujibu wa mpenda ubuyu wetu ambaye naye alikuwemo ukumbini humo, kwa kumtazama Aunt anaonekana kuwa na ujauzito wa si chini ya miezi minne sasa na kwamba Wema ambaye ni shosti wake anadaiwa kuwa huwa anamsindikiza kliniki lakini staa huyo ameendelea kusisitiza kuwa hana.

UJAUZITO MIEZI MINNE
“Mimi najua muda mrefu na jinsi anavyoonekana kwa sasa hakuna ubishi kwani ujauzito wake una kama miezi minne hivi,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:SOMA ZAIDI>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname