21 December 2014

HUYU NDO WAZIRI ALIYE WEKA PICHA MTANDAONI HUKU AKIWA KAVAA BIKINI

Picha aliyopost Instagram Waziri wa Vijana na Utamaduni (Youth and Culture Minister) wa Jamaica, Lisa Hanna, imezuagumzo na malalamiko. Baadhi ya wananchi wa Jamaica wamefunguka katika mitandao ya kujamii wakisema kuwa ni kinyume cha maadili na udhalilishaji wa nchi yake kwa waziri kupost picha akiwa nusu-uchi.
Picha hiyo inayodaiwa kupigwa na mwanae Alexander Panton 
baada ya Reggae Marathon, inamuonyesha mwanasiasa huyo 
akiwa beach, amevaa yellow two-piece bikini na fulana yenye picha 
ya marehemu Bob Marley
Lisa Hanna jamaican minister miss world swimsuit breaks jamaica Waziri azua gumzo, alaaniwa kwa kupost picha akiwa amevaa bikini
Picha aliyopost Waziri wa Vijana na Utamaduni wa Jamaica akiwa ndani ya bikini, iliyozua gumzo na kulaaniwa na baadhi ya wananchi wa nchi hiyo
Lakini kwa msiomjua, waziri Lisa Hanna si mwanasiasa wa kawaida, kwani alikuwa Miss Jamaica, na alitwaa taji la Miss World 1993. Enzi zake alikuwa ni mmoja wa warembo wakali kuliko duniani, na hata sasa ni bado mkali.
Lisa Hanna jamaican minister miss world swimsuit Waziri azua gumzo, alaaniwa kwa kupost picha akiwa amevaa bikini
Hii si mara ya kwanza kwa waziri Hanna kupost picha ya swimsuit. Miezi mitano iliyopita alipost picha hii; lakini tofauti ni picha hii aliipiga miaka 10 iliyopita, kabla ya kuingia kwenye siasa

Baadhi ya Wajamaica, akiwemo Senator wa kike Marlene Malahoo Forte, wamemtetea waziri huyo wakisema kivazi alichovaa ni muafaka kwa beach.
Waziri Lisa Hanna mwenyewe hajatoa kauli yoyote kuhusu ishu hiyo na anaendelea kupost picha Instagram na raha zake. Vipi unaonaje? Amechemsha au ni sahihi?
Lisa Hanna jamaican minister miss world Waziri azua gumzo, alaaniwa kwa kupost picha akiwa amevaa bikini
Mrembo huyo ni mmoja ya wanasiasa walio busy Instagram. Hapa anachukua “selfie”
Lisa Hanna jamaican minister miss world1 Waziri azua gumzo, alaaniwa kwa kupost picha akiwa amevaa bikini
Akiwa saloon akisubiri kutengenezwa nywele, huku akikuonyesha kinyemela kuwa usafiri bado wamo
Lisa Hanna jamaican minister miss world2 Waziri azua gumzo, alaaniwa kwa kupost picha akiwa amevaa bikini
Ni mmoja wa wanasiasa wakali katika “high-fashion.” Of course alishawahi kuwa Miss World, hivyo lazima a-represent

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname