Leo hii Shetta ameonyesha kusikitishwa na kitendo hicho na kujitetea kuwa alipigiwa simu na mtanagzaji mmoja na kumuuliza kuhusu collable yake na alikina na ndipo aliposhtuka na kusema yeye hana colable na Alikiba na wala saa hii hana mpango wa kuwa na collable na msanii yoyote wa ndani wala wa nje
“Alikiba mi sina tataizo nae kabisa wala msanii
yoyote Tanzania, lakini kitu ambacho nimekiona tangia jana na leo kwenye
baadhi ya bogs na habari tofauti tofauti kwamba “angali shettah
alichojibu baada ya kuulizwa collable na Alikiba” kwanza nianzie kwenye
hiyo story, niliulizwa kwamba kuhusu collable lako na Alikiba, mi nikawa
nimeshtuka sababu sina collable na Alikiba na sijafanya yaaani kabisa
collable na Alikiba lakini nilichokijibu ni kwamba “Sijafikiria kufanya
wimbo na msanii yoyote Tanzania kwa sasa hivi , nikatoa sababu, sababu
nimefanya collable nyingi sana hapa ndani, kwahiyo nilichokijibu ni
kwamba kiroho safi tu kwamba sifikirii kufanya kazi na msanii wa ndani
labda nifanye na international artist kwasababu labda ya kunisongeza
zaidi zaidi mbele au nifanye wimbo peke yangu,” amesema Shettah
Ofcourse kama inafika time nahitaji kufanya kazi
na Alikiba na yeye yupo willing tutafanya wimbo, ameendelea kuongea
Shettah, lakini sijawahi kuhit au kutoka katika mziki wngu kwa kumsema
mtu vibaya au kujaribu kuzungumza kitu kibaya ili ije iwe story watu
wazungumze, kwahiyo nilichokijibu nilikuwa sawa kutokana na swali
nililoulizwa, kwahiyo baada ya kuja kugeuka na zile headline
zilizoandikwa kwenye blog mbalimbali, watu kuja kunitukana kuzungumza
vibaya kwenye social network, kwenye page yangu, imekuwa tatizo, kwangu
mimi si kitu kizuri yaani haijakaa vizuri kwa upande wangu.
No comments:
Post a Comment