08 November 2014

MWANADADA ACHINJWA KINYAMA NA KUNYOFOLEWA SEHEMU NYETI

Watu wasiofahamika wamemuua kwa kumkata mapanga na kisha kumnyofoa sehemu zake za siri mkazi wa Kijiji cha Kanegele, wilayani Mbogwe, Mkoa wa Geita, Hollo Machibula (54).
Akizungumza kijijini hapo juzi, Diwani wa Kata ya Bukandwe, Henry Alphonce alisema Hollo alivamiwa na watu hao nyumbani kwake juzi saa 5:00 usiku akiwa amelala na kuanza kumkatakata kwa mapanga.Alphonce alisema mwanamke huyo alikuwa akiishi na binti yake, Tatu Juma (25) ambaye wauaji hao walimlazimisha kuingia chini ya uvungu wa kitanda kabla ya kuanza kumshambulia mama yake.Alisema alipata taarifa za tukio hilo saa 6:00 usiku baada ya kupigiwa simu na viongozi wa kitongoji waliofika eneo la tukio na kushuhudia mauaji hayo.

Mtoto huyo alisema alishuhudia jinsi mama yake alivyokuwa akichinjwa na kunyofolewa sehemu zake za siri walizotoweka nazo wauaji SOMA ZAIDI>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname