Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ akitafakari jambo. Ishu hiyo iliyojaa utata mkubwa, ilitokea saa nne usiku maeneo ya Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam kwenye barabara inayotoka barabara kuu kwenda kanisani kwake.
NI kama kimenuka tu! Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar, Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ usiku wa kuamkia Jumatatu iliyopita alizua la kuzua kufuatia kumimina risasi kadhaa hadharani kwa madai ya kuwatawanya kundi la vijana waliodaiwa kumvamia na kuziba barabara kwa lengo la kumfanyia kitu mbaya.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, tukio lilianza kwa Mzee wa Upako aliyekuwa akipita kwa miguu kukejeliwa na vijana waliomwita Freemason kauli ambayo mtumishi huyo wa Mungu aliiona ni ya kejeli kwake.“Baada ya kuitwa Freemason, yule kijana akiwa na wenzake waliendelea kumkejeli Mzee wa Upako, akawafuata na kuwauliza mbona mnanitukana, nimewakosea nini?”
“Alipoona wale vijana wanazidi kumkejeli huku wakionesha dalili za kumfanyia fujo ndipo alipotoa bastola yake na kufyatua risasi tatu juu hali iliyowafanya wale vijana kutawanyika huku na kule.
“Baadhi ya watu walikuwa kwenye biashara zao, nao walitimua mbio, wengine waliacha biashara, unajua risasi ni risasi tu, mtu akisikia risasi hawezi kukaa salama hata kama ni mjeshi,” kilisema chanzo hicho.SOMA ZAIDI>>>
No comments:
Post a Comment