09 November 2014

INASHANGAZA NA KUSIKITISHA SANA HUYU NDIO MTOTO ALIYEZALIWA ANASEHEMU ZA SIRI 4



AGANO kwamba nyakati za mwisho, matukio mengi ya ajabu yatadhihirika, linazidi kupata nguvu kutokana na tukio la kusikitisha lililotokea Arusha.

Wakazi wa jiji hilo, wanaliita A-Town na ukifanikiwa kushiriki vijiwe mbalimbali, utabaini jinsi mkoa huo ulivyozizima kutokana na kuzaliwa motto mwenye sehemu nne za siri.
Kila kona ya jiji hilo, anazungumzwa mtoto huyo kwa hali ya mshangao. Malaika huyo wa Mungu hajapewa jina lakini mama yake anaitwa Naishooki Logolie, 23, mkazi wa Kijiji cha Injok, Wilaya ya Arumeru, Arusha. 
Kutokana na habari ya mtoto huyo kupata umaarufu mkubwa, huku wengi wakitaka kumjua zaidi, Uwazi lilimsaka mtoto huyo na kubaini maajabu mengine kwamba mbali na sehemu hizo za siri pia ana miguu mgongoni.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname