31 October 2014

MUHUBIRI ALIYESEMA MATAULO YA KENYA YANA UKIMWI AOMBA RADHI

Kituo kimoja cha televisheni nchini Marekani kinachorusha kila siku kipindi cha mhubiri Pat Robertson kiliomba radhi Jumatatu kwa madai yake potofu kwamba wasafiri wanaokwenda Kenya wanaweza kupata maambukizi ya Ukimwi kwa njia ya taulo.
"Dr Robertson alikosea kusema juu ya uwezekanao wa kupata Ukimwi kwa njia ya mataulo," kimesema kituo cha Utangazaji cha Kikristo, CBN, katika mtandao wa Facebook.
"CBN imegundua mara moja kosa hili na kuondoa kauli hiyo kutoka kwa maktaba ya mtandao huo. CBN inaomba radhi kwa mkanganyiko wowote."
Mhubiri huyo mwenye umri wa miaka 84, mwinjilisti mkongwe ameonya katika kipindi chake cha "700 Club" cha Oktoba 16 kwamba wasafiri watalazimika kuchukua tahadhari ya hali ya juu ya kiafya wawapo nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname