Fumanizi huupasua moyo na kuumiza misuli yote ya mwili kiasi cha kupampu kwa nguvu zote sumu ya hasira iliyo mwilini mwako. Lakini huu ndio wakati ambapo ukizifuata hisia zako unaweza kufanya maamuzi ambayo utayajutia maisha yako yote pindi hasira hizo zitakapozimika.
Amani Misana, mtangazaji wa kipindi cha Pillow Talk cha 100.5 Times FM na mtaalam wa masuala ya mahusiano ya ndoa amependekeza adhadu bora zaidi inayofaa kumpa mpenzi wako itayayobadilisha kabisa moyo na saikolojia yake bila wewe kuingia matatizoni.
“Japo naweza kuonekana kama nina kichaa vile, lakini ukweli ni kwamba njia bora ya kumu adabisha mpenzi wako anaekusaliti ni kumpenda zaidi badala ya kumdhuru au kujidhuru wewe mwenyewe.”Amesema Amani Misana kwenye maelezo yake.
“Kumbuka aina yoyote ile ya kudhuru madhara yake ni lazima yarudi kwako kwa njia moja ama nyingine lakini pia uliyempenda kwa ukweli huwezi kumdhuru kwani falsafa ya upendo wa kweli inasema pendaneni kwa wema hata kama mtaachana basi achaneni kwa wema. Kwa kuwa mapenzi ni wema.” Ameongeza.
No comments:
Post a Comment