Densi ya kunengua viuno na tumbo ya 'Belly Dance nchini Misri
Bodi
ya kidini ya misri, imetoa fatwa kukataza uonyeshaji wa kipindi
kilichoanzishwa kwenye televesheni nchini humo kuonyesha densi ya jadi
ya wanawake wa misri ya kunengua viuno almaarufu 'belly dance'.
Ngoma
hiyo inayofanana na chakacha ya waswahili imechezwa tangu zama za kale
na imenakiliwa hata katika enzi za ma-pharoah katika nchi hiyo ya
Misri.Maelfu ya watalii wanaoitembelea Misri hupenda kwenda kuona
inavyochezwa lakini mnamo siku za hivi karibuni wasichana kutoka sehemu
nyingi duniani hasa ulaya na hata uchina wameripotiwa kwenda Misri
kujifundisha jinsi ya kucheza densi hiyo.Ni densi ambayo isingekosekana
kwenye sherehe muhimu. Harusi au burudani nyenginezo.
Ni ajabu kuwa sasa imekuwa maarufu katika mataifa ya kigeni kuliko Misri kwenyewe ambako haichezwi ovyo ovyo hadharani.
Misri
ni nchi ya waislamu wengi hivyo burudani zina miiko yake- densi kama
hizo hazichezwi hadharani hasa kwenye mikusanyiko ya umma ya
mchanganyiko wa wake kwa waume.
Hivi
wale wanaozishabikia ni wachache kiasi kuwa sasa kuna hofu kuwa huenda
utamaduni au ustadi huo wa belly dancing unakufa polepole Misri.
Pengine
ni kwa kutambua hilo ndio waandalizi wa vipindi wakaona bora walete
shindano la ngoma hiyo kwenye televisheni ya kitaifa kuhifadhi na kuipa
umaarufu kama kitu cha asili ya Misri.
Lakini bila shaka hilo haliswihi machoni pa bodi ya kidini nchini humo na wametoa amri kipindi hicho kiondolewe mara moja .
Bodi
hiyo Dar al-Ifta imesema kuonyesha watu wakinengua viono kwenye
televisheni kutazorotesha maadili ya jamii na kutapelekea mwenye itikadi
kali kupata visababu vya kuipaka matope Misri ili kutia doa imani ya
kiislamu ya taifa hilo.
Kutokana na kauli hiyo sasa kipindi kilichoikuwa kipeperushwe hewani juzi usiku kimeahirishwa.
Ni
makala moja tu ya kipindi hiyo ndiyo iliyooneshwa - Mojawapo wa
waliokuwa majaji wa kupendekeza washindi kwenye kipindi hicho ni
mchezaji maarufu wa densi hiyo aitwae Dina na wengi wa washindani katika
mchuano huo wa belly dancing wala si raia wa Misri
No comments:
Post a Comment