03 September 2014

DEREVA WA BODABODA MOSHI ASHINDA TIKETI KUHUDHURIA FAINALI YA SERENGETI FIESTA DAR

Dereva wa bodaboda mjini Moshi amepata fursa ya kukutana na msanii wa kimataifa siku ya fainali za Serengeti fiesta zitakazo fanyika Oktoba 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam baada ya kushinda katika shindano la “ni sheedah moment”linalofanyika katika mitandao ya kijamii ya Facebook na twitter.

Akizungumzia kushiriki kwake katika shindano hilo ambapo mshiriki hutuma picha katika uwanja wa twitter na facebook, Bwana Nikolaus alisema kwamba baada ya kusikia tangazo redioni, alitumia fursa hiyo kutuma picha yake akifurahia bia ya Serengeti Premium lager na kuituma katika twitter.
Masaa kadhaa baadae alipigiwa simu na wahusika kutoka Serengeti breweries na kumtangaza kama mshindi. “Sikuamini…nilishangilia kwa furaha sana hasa ukuzingatia kwamba imekuwa ndoto yangu ya muda mrefu kukutana na msaanii toka nje ya nchi…ninatamani siku ifike mapema,” alisema Nikolaus.
“Hii ni mara yangu ya kwanza kushiriki shindano hili, na ninaishukuru sana kampuni ya Serengeti kwa kunipa fursa ya kwenda Dar es saaam kushuhudia fainali za Serengeti Fiesta 2014 ” aliongeza Bwana Nikolaus.
Mshindi huyo alitoa wito kwa vijana wenzake kushiriki katika shindano hili ili nao wapate fursa ya kwenda kushuhudia fainali za Serengeti fiesta.
Shindano la ni sheedah moment linaendeshwa na kampuni ya Push Mobile Media Limited katika mitandao ya kijamii facebook na twitter, ambapo kwenye Facebook mshiriki atumie link hapa chini kuweza kujisajli kwenye shindanohttps://www.facebook.com/serengetipremiumlager/app_739696419428430 na kwa wale wa twitter mshiriki atume picha kwenye ukurasa wake yenye hashtag #nisheedahmoment
Washindi watazawadiwa zawadi mbalimbali ikiwemo bidhaaa mbalimbali za Serengeti, baadhi ya washindi hawa pia watapata fursa ya kushinda tiketi ya kuhudhuria fainali za Serengeti fiesta mjini Dar-es salaam ambapo msanii wa kimataifa atatumbuiza.
Baada ya Moshi, joto la Serengeti fiesta linaendelea kusambaa katika mikoa mbalimbali hapa nchini na baadae kumalizia jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname