Waigizaji wakongwe kwenye tasnia ya
filamu Bongo, Jacob Steven ’JB’ na Vincent Kigosi ‘Ray’ wamempigia
saluti muigizaji mwenzao, Kajala Masanja kutokana na filamu fupi
aliyotengeneza ya Mbwa Mwitu.
“Kitu ambacho nimekipenda ni kwamba
filamu ni fupi lakini ujumbe umeeleweka pia amefikiri kitu cha tofauti
kabisa kwani hata watoto wa rika zote wanaweza kuangalia kwa ajili ya
kujifunza,” alisema JB huku Ray akiunga mkono hoja.
No comments:
Post a Comment