the QUARTZ Blog
Kwa bahati mbaya hakutakuwa na toleo safi la video hiyo ambayo kila sekunde yake ina mengi.
Akiongea na Nick Martinez katika mahojiano maalum kabla ya kuachia rasmi video hiyo, rapper huyo ameeleza kuwa hajui ni jinsi gani anaweza kufanya toleo safi la video ya wimbo huo.
“Nilikuwa nasema tangu awali kuwa sijui ni jinsi gani ntakuja kufanya clean version (safi kimaadili) ya hii video.” Amesema Nicki Minaj.
Rapper huyo pia alizungumzia ujumbe aliolenga kuufikisha kwa wasichana wenzake kama msanii kupitia video hiyo.
“Moja kati ya vitu ambavyo nilitaka kufanya na huu wimbo ilikuwa kupeleka ujumbe kwamba kuwa na makalio makubwa au madogo (sio tatizo)….najua kwa sababu mimi niko kwenye biashara, niko kwenye pressure ya kuwa mwembamba sana, unajua kwa kweli nataka kupungua uzito hata sasa hivi.
“Lakini sitaki kutuma ujumbe kwa wasichana wengine kuwa sio kila wakati wanapoangalia kwenye TV wataona mtu wa ‘kijamii’ kwa sasabu sio uhalisia.” Alieleza.
Ameongeza kuwa aliamua kutoa ‘cover’ ya aina ile ikionesha makalio makubwa kwa sababu huona models ambao ni wembamba sana na huonesha makalio yao mara nyingi lakini haionekani kama ni kitu cha ajabu.
No comments:
Post a Comment