BAADA ya kutua nchini, kocha wa Simba Patrick Phiri alishtuka
kusikia Mbrazili Marcio Maximo yupo Yanga na sasa jamaa amemjibu Phiri
akisema: “Ndio nipo Yanga nimejaa tele.” Akaendelea na mambo yake.
Maximo amesema ushindani mkubwa wa namba ulioko
kwenye kikosi cha klabu hiyo umewafanya baadhi ya wachezaji wanaougua
malaria kutaka kuendelea na mazoezi badala ya kupumzika.
“Namfahamu kocha Phiri (Patrick), ni kocha mzuri,
nilifurahi kufanya naye kazi kipindi nikiwa timu ya Taifa na yeye akiwa
Simba, nina imani kuwa ujio wake utaongeza changamoto kwenye ligi na
ubingwa utakuwa mgumu zaidi msimu ujao,” alisema Maximo
Akizungumzia wachezaji wake, Maximo alisema:
“Ushindani wa namba kwenye kikosi changu umekuwa mkubwa, nafarijika
kuona kila mchezaji anataka kucheza, hiyo inanipa imani kuwa nitakuwa na
kikosi bora msimu ujao.”
No comments:
Post a Comment