Stori: Gladness Mallya
WAMEMALIZANA! YOBNESH Yusuph ‘Batuli’
anayekimbiza kunako soko la Bongo Movies, amefunguka kuwa hataki kusikia
habari za aliyekuwa mpenzi wake aliye pia msanii mwenzake, Mtunisi
kwani mapenzi yalishaisha.
Akistorisha na paparazi wetu, Batuli
alisema hataki kumsikia wala kujua habari za Mtunisi kwani mapenzi
yalikuwa zamani lakini kwa sasa kila mtu ana maisha yake yaani yeye
Mtunisi ana mke na yeye ana mpenzi wake.
“Mimi kwa sasa nina maisha yangu na
Mtunisi ana maisha yake nawashangaa wanaoniandama kwa maneno kwamba bado
niko naye, jamani Mtunisi ana mke na mimi nina mpenzi hivyo sitaki
kusikia habari hizo kabisa,” alisema Batuli.
.jpg)
No comments:
Post a Comment