Alikiba anataka watu wafahamu kuwa hana na tatizo na Diamond Platnumz na amewataka watu waache kuwakosanisha.
AliKiba amewataka watu kuachana na tabia ya kuwagombanisha Diamond ili wafanye muziki mzuri.“Kila mtu anaandika anachotaka juu ya mimi na Diamond, mpaka wengine wanatumia akaunti fake za Facebook kutukosanisha, ndio maana nikasema kuna wengine wanafanya for fun na wengine wanafanya ili kutukosanisha wengine wanafanya lakini hawajui wanachofanya,” amesema Alikiba.“Mimi najaribu kuwaomba wadau mbalimbali waache hiyo tabia ya kutukosanisha kwa sababu mimi sina ugomvi na Diamond na wala sina mambo hayo. Ninachowataka waendelee kusupport kazi zetu ili mambo yaende vizuri kwa sababu sisi ndo wasanii wao tunaoiwakilisha Tanzania. Wanapotupa moyo wao sisi tunazidi kukaza buti ili tufike mbali zaidi. Watu wanaotengeneza ugomvi wangu na Diamond waache cha zaidi wafanye kusupport muziki na watuambie ni mapungufu gani ambayo yamepungua ili tujirekebishe,”SOMA ZAIDI>>
No comments:
Post a Comment