02 July 2014

Pistorius katika hatari ya 'kujiua'


Meneja wa Pistorius anasema anaomboleza kifo cha mpenzi wake

Ripoti ya daktari wa magonjwa ya akili iliyowasilishwa katika kesi dhidi ya Mwanariadha mashuhuri Afrika kusini, Oscar Pistorius, inaashiria kuwa anaugua msongo wa kimawazo na yumo katika hatari ya kujitoa uhai.
Ripoti hiyo iliyowasilishwa na wakili wake, inasema anamuomboleza mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Siku ya Jumatatu, mahakama ilielezwa kwamba Pistorius hana matatizo ya akili wakati alipompiga Bi. Steenkamp risasi .

Anakana kutekeleza mauaji hayo, akieleza kuwa ilikuwa bahati mbaya alipohofia kwamba aliingiliwa nyumbani mwake na mtu asiyemjua.
Awali meneja wa Pistorius alihojiwa.
Ufanisi wa Pistorius
Siku ya Jumanne, Peet van Zyl alisema Pistorius amekuwa mtu anayejulikana kimataifa katika mashindano ya olimpiki kwa walemavu ya mwaka 2012, na alitarajiwa kufanikiwa zaidi.
Mwanariadha huyo aliyekatwa miguu yake miwili, alishindana katika mashindano hayo ya walemavu na ya olimpiki huko London.
Van Zyl amesema huenda Pistorius angejiongezea kipato chake mara tano au sita zaidi.
Aliongeza kwamba ni mfanyabiashara na ana nafasi nyingi kutokana na kusifika kwake.
Mwandishi wa BBC anasema Pistorius akiwa kizimbani Pretoria, ni hakika kwamba aliyatafakari yaliokuwa yakisemwa na Van Zyl kuhusu uwezekano wake kufanikiwa zaidi ambao kwa sasa umebadilika.
'Ombi kusitisha vikao'
Mwendesha mashtaka Gerrie Nel amesema hakujuwa kwamba Van Zyl angeitwa mahakamani kutoa ushahidi na ameomba mahakama isitishe vikao hadi Jumatano ili ajitayarishe kumhoji, ombi ambalo jaji aliliridhia.
Bwana van Zyl ni miongoni mwa mashahidi wa upande wa utetezi kuwasilishwa.
Mwandishi wetu anafahamu kwamba huenda upande wa mashtaka baadaye ukamuita daktari huyo, aliyemchunguza Pistorius katika mwezi uliopita, aje atoe ushahidi
Madaktari watatu wa mgonjwa ya akili waliiwasilisha ripoti moja iliyosema mwanariadha huyo yupo sawa kiakili kuendelea na kesi yake

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname