Thursday, 10 July 2014
KUHUSU USHIRIKI WA ADAM KUAMBIANA KWENYE VIDEO YA MDOGO MDOGO YA DIAMOND
Ni
kitu ambacho hakuna mtu ambaye aliwahi kuhisi au kutegemea kama
Marehemu Adam Kuambiana ambaye alikua muongozaji[Director] wa filamu
nyingi za Kitanzania kumbe nae kashiriki kwenye video ya Mdogo Mdogo.Adam Kuambiana ambaye alifariki May 17 2014 wakati akiwa kambini kwa ajili ya filamu yake mpya ametajwa na Diamond kuhusika na utengenezaji wa Script[muongozo] wa video ya Mdogo Mdogo iliyotengenezwa South Africa na God Father.
Diamond
ameongea na XXL na kusema>>’Script wakati inaanza nilikua kama
natamani nifanye kitu fulani lakini nilikua sijui naanzaje sasa
nakumbuka kipindi hicho Adam Kuambiana walikuwa wana shoot na kuongoza
movie ya wakina baby[Wema] mimi nilipokua naenda kambini nakutana naye’‘Baby alinambia ni mzuri sana nikamfata nikamwambia nina nyimbo yangu nataka uniandikie stori wimbo wangu unaenda hivi na hivi akanambia ni vizuri nikifika studio niisikilize kwanza huo wimbo’
‘Nikawa nae studio nakumbuka nilikuwa nae studio kwa Tudd Thomas pale THT akawa anasikiliza wimbo akawa ananambia namna stori inavyotakiwa kwenda so naweza kusema stori inavyoanza picha hata ya kupata Stori ni Kuambiana ndiye aliyenipa.
No comments:
Post a Comment