25 May 2014

VIONGOZI WA MBWA MWITU NA PANYA ROAD WATIWA MBARONI DAR

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata viongozi sita wa makundi ya uhalifu maarufu kwa majina ya Mbwa Mwitu na Panya Road.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi wa kanda hiyo, Suleiman Kova, aliwataja viongozi hao kuwa ni Athumani Said (20), Joseph Ponela, Clement Petter (25) na Romans Vitus (18) wakazi wa Kigogo.Wengine ni Mwinshehe Adamu (37) mkazi wa Temeke na Daniel Petter (25) mkazi wa Yombo, huku kamanda huyo akibainisha kwamba maeneo yenye vijana hao wahalifu ni Kigogo, Magomeni, Tabata, Manzese na Mbagala ambapo askari wa kutosha wapo kwa lengo la kuwadhibiti.SOMA ZAIDI HAPA >>>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname