24 May 2014

ULEVI NI NOMA! JANKI AFA KWA KUZIDISHQA MITUNGI

Mwili wq ‘janki’ Geoffrey Mlelwa ukiwa kwenye gari la polisi

MBALI ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na makampuni ya kutengeneza pombe kutoa tahadhari kuwa unywaji wa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya, ‘janki’ Geoffrey Mlelwa (26), mkazi wa Ipogolo mjini hapa, amejikuta akiyakatisha maisha yake kwa kudaiwa kugida pombe kupindukia.Tukio hilo la kusikitisha lilijiri juzikati ambapo kijana huyo alikuwa katika Soko Kuu la Manispaa ya Iringa akiwa na wenzake wakipiga ulabu kwa staili ya kuchanganya (kuchoma sindano) ndipo Geoffrey alipopitiliza na kusababisha apoteze uhai.
Wakizungunza na mwanahabari wetu, baadhi ya mashuhuda walidai kuwa kijana huyo enzi za uhai wake alikuwa ni mtu wa kunywa pombe za kienyeji aina ya ulanzi na bangi ila siku hiyo alionekana mwenye ‘mihela’ hivyo kuachana na kunywa pombe aliyoizoea na kuanza kunywa pombe ya kisasa kama grants, viroba na kuchanganya na ulanzi ndani ya chupa moja.
“Mbali ya ‘kuchanganya madawa’, kijana huyo hakula chakula chochote tangu alipoanza ‘kupiga vyombo’ na alipozidiwa, rafiki yake alimkokota na kumpeleka chumbani kwao (geto) kabla ya asubuhi kuamka na kumkuta amekufa,” alisema shuhuda mmoja kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini.Soma zaidi>>>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname