23 May 2014

Ebwana umesikia hii ya Iran? Polisi wamekamata waliojirekodi video ya ile happy ya Pharrel


Hit single ya ‘happy’ ya Pharrell Williams ni single ambayo ukiangalia kwenye mtandao watu wengi walitengeneza video zao na kuziweka humo lakini kwa kutumia wimbo huohuo ambao kiukweli wanasema ni wimbo uliovunja rekodi kwenye nchi ambazo hata hakuwahi kuifikia hiyo rekodi.

Kama ilivyotokea kwa mataifa mengine, mashabiki sita wa Pharrell nchini Iran waliamua kutengeneza video yao wakiwa ni wasichana na wavulana na baada ya kuirekodi wakaiweka kwenye mtandao.

Iran ikiwa ni nchi ambayo ina sheria zake kazi ikiwemo za dini zinazobana, iliwachukulia hatua kwa kuwakamata wote sita walioonekana kwenye video hiyo ambapo mkuu wa Polisi Tehran Hossein Sajedinia alithibitisha hilo na kwamba baada ya video kusambaa walianzisha uchunguzi uliofanikishwa watu hao sita kukamatwa baada ya saa sita.

 
Mkuu huyu wa Polisi amewaonya vijana wa Iran kwamba yeyote atakaekwenda kinyume na taratibu au kanuni za nchi na dini atakamatwa kama ilivyotokea ambapo CNN walisema moja ya makosa yaliyofanya watu hao kukamatwa wakiwemo wasichana ni kucheza kwa kushikana na pia kuacha wazi nywele na sehemu nyingine za mwili.
Baada ya watu hawa kukamatwa walikiri kwamba haikua lengo lao kuiweka hiyo video online ambapo mwingine alisema walitokea kwenye video ikiwa ni sehemu ya mazoezi ya kuigiza kwenye TV.

Baada ya kukamatwa kwa watu hao sita Mwandishi wa habari wa Iran Golnaz Esfandiari aliandika ‘Iran ni sehemu ambayo ukiwa na furaha unakamatwa’

Hii ni tweet ya Pharrell akielezea masikitiko yake

Hata hivyo taarifa za saa kadhaa zilizopita zinasema watu hawa inaaminika wameachiwa kwa dhamana baada ya kuchukua headlines iliyoanzia kwenye kituo cha taifa cha TV ambapo walihojiwa camera zikichukua picha kutoka migongoni mwao, yaani hawakuonekana sura.

Mmoja wa sita hao walikua wameshikiliwa aitwae Taravati alipost kwenye Instagram na kummention Pharrell kwa kusema ‘hI, nimerudi… asante sana Pharrell na kila mmoja alietujali nawapenda wote sana na niliwamiss

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname