KAUNTA INAENDELEA KUPANGWA VITU
BAADHI YA SEHEMU ZA KUTULIA
NURMAK KWA AJILI YA KAZI MOJA YA BURUDANI
Dj ABUU FRESH Jr WA THE CLUB HOUSE AAHIDI VITU VIPYA KWA WAKAZI WA MUSOMA
MWANAMUZIKI ANAYEKUJA KWA KASI HAPA NCHINI SHILOLE "SHISH BEBY KESHO ANATARAJIWA KUTOA BURUDANI YA AINA YAKE KWA WAKAZI WA MJI WA MUSOMA IKIWA NI UZINDUZI RASMI WA UKUMBI WA KISASA WA THE CLUB HOUSE BAADA YA KUFANYIWA UKARABATI WA NGUVU.
AKIZUNGUMZA NA BLOG NDANI YA UKUMBI HUO,DJ MKUU WA CLUB HIYO ABUBAKAR NYAMAKATO DJ ABUU FRSH Jr AMESEMA MAANDALIZI YOTE YAMEKWENDA VIZURI KILICHOBAKI NI WAKAZI WA MUSOMA KUPATA BURUDANI YA AINA YAKE.
AMESEMA SHILOLE AKIWA NA KUNDI LAKE ZIMA LA WACHEZA SHOW AMEIPANIA SHOW HIYO KWA KUFANYA VIZURI ILI KUJENGA JINA ZURI KWA MASHABIKI WAKE AMBAO KWA KIASI KIKUBWA WAMETOKEA KUMUUNGA MKONO.
Dj ABUU AMESEMA KIINGILIO KWENYE SHOW HIYO YA AINA YAKE ILIYODHAMINIWA NA WADAU MBALIMBALI WA BURUDANI IKIWEMO BROG HII KITAKUWA SHILINGI 7000 HUKU SHOW IKITARAJIWA KUANZA MAPEMA SAA 2 USIKU NA KUOMBA WAPENZI WA BURUDANI KUJITOKEZA KWA WINGI
No comments:
Post a Comment