Star
wa filamu nchini Vicent Kigosi "Ray" amesema kuwa yeye ana pesa na mali
nyingi na hakuna msanii yeyote wa Tanzania awe wa filamu au muziki
anayemfikia sema hapendi tu kujitangaza kama baadhi ya mastaa wenzake
akidai ni ulimbukeni. "hakuna msanii anayenizidi uwezo kuanzia mali na
hata fedha niko mbali sana mimi, hata gari ninalotembelea hakuna msanii
aliyenalo kama ingekuwa ni mtu wa kujisifusifu na kutafuta sifa za
kijinga jamii ingejua" alisema star huyo wa filamu za Oprah, Sobbing
Sound, Hard Price na Handsome Wa Kijiji akizungumza na gazeti moja.
Ray
vile vile aliamua kurusha kombora kwa wabaya wake wasiopenda maendeleo
yake kwa kusema "wanaongea sana majungu, fitina na vitu ambavyo havipo
kuhusu mimi, mimi ni jembe, kwanini wasiangalie maisha yao? leo msanii
unateta nae dakika hiyo hiyo anageuza maneno hayo kuwa majungu, acha
nikae peke yangu nifanye issue zangu"
No comments:
Post a Comment