Mwili wa marehemu uliwasili kwa ndege ya K.L.M saa 4 kasoro robo usiku wa jana, huku baadhi ya wadau wa muziki na wanandugu wakionesha kushangazwa na kitendo cha baadhi ya wanamuziki kutokufika katika kuupokea mwili wa Amina Ngaluma.
Kamera yetu ilishuhudia wasanii wachache waliowasili eneo la Uwanja wa Ndege akiwemo Mzee Cosmasi Chidumule na Mwijuma Muumini ambaye alitoka Kahama kwa ajili ya kuudhuria mazishi ya mwanamuziki huyo anayetarajiwa kuzikwa leo mchana.
No comments:
Post a Comment