01 May 2014

MR BLUE: WEMA, NAJMA WALINIFILISI

NYOTA wa Bongo Fleva, Herry Samir maarufu kama Mr. Blue amesema wasichana warembo, Wema Sepetu na Najma ambao aliwahi kutoka nao kimapenzi kwa nyakati tofauti miaka ya nyuma, walimfilisi kutokana na matumizi makubwa ya fedha alipotoka nao viwanja.
 
Nyota wa Bongo Fleva, Herry Samir maarufu kama Mr. Blue akiwa kwenye pozi.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Mr. Blue, msanii aliyeanza kupata umaarufu akiwa bado kijana mdogo, alisema alilazimika kutumia fedha nyingi akiwa nao, kwani vinginevyo wangemuona hana pesa, kitu ambacho hakuwa tayari kuona kinatokea.
“Mademu wengi walikuwa wanapenda sana starehe, kila day (siku) wanataka twende kiwanja, ndiyo maana kama unakumbuka niliyumba kimuziki.


Wema Sepetu a.k.a 'Beautiful Onyinye'.
“Wanawake wengi niliotoka nao hawajulikani, ila kuna Wema na Najma, ilikuwa ukizama nao dukani lazima ufanye shopping (manunuzi) ya nguvu, kuanzia laki saba, nane na kuendelea ili wakuone unazo na mademu wengi wakisikia tu umepiga shoo, sms hazikauki kuomba uwatumie mawe (pesa),” alisema.
Kuhusu maisha yake ya sasa, Mr. Blue alisema yamebadilika sana, kwani hivi sasa ameoa mwanamke mwenye asili ya Kiarabu na amejaliwa kupata mtoto mmoja, hivyo ni baba wa familia ambaye pia anakaribia kumaliza mjengo wake siku si nyingi.

Mrembo Najma.
Hata hivyo alisema mkewe siyo maarufu, ana malengo na upendo kwani amekuwa akimuaga kila safari anayofanya na kwamba hata yeye anaporejea nyumbani, hupokelewa vizuri.
Mr. Blue ni mmoja kati ya wasanii wa muda mrefu ambao bado wanafanya muziki na wenye mashabiki wengi ndani na nje ya Bongo.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname