21 May 2014

FISI WAKUTWA NA SHANGA NA ROZALI KIUNONI.

MSAKO wa Fisi waliovamia makazi ya Vitongoji vitatu vya Kijiji cha Hungumalwa Kata ya Hungumarwa wilayani Kwimba mkoani Mwanza, umezua maajabu.
Maajabu hayo yamehusishwa na imani za kishirikina, baada ya fisi wawili kati ya 12 waliouawa, kukutwa wamevalishwa shanga na Rozali, kiunoni.
 Msako huo wasiku tatu ulioanza juzi(Jumapili) unahusisha mamia ya wananchi wa Kijiji hicho na vitongoji vyake vya Mwanzabalemi, Mwanega na Mwang’ombe, wanaotumia siraha za jadi na mbwa wapatao 50.
Habari za ndani kutoka Kijijini humo zimesema kwamba, kabla ya wananchi hao kuingia ‘vitani’ kusaka wanyama hao ambao baadhi wanadaiwa kumilikiwa na watu wachache wanaojihusisha na vitendo vya ushirikina, wazee wa Kijiji na Vitongoji hivyo, walifanya mazindiko (kinga) ya kujikinga na nguvu za washirikina ambazo zinge kwamisha zoezi hilo.Soma zaidi >>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname