Tukiwa bado na Majonzi ya Kifo cha Adam Kuambiana,msanii mwingine afariki Dunia leo Hospitali ya Taifa Muhimbili

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSANII
wa filamu hapa nchini, Adam Kuambiana, pichani juu, anatarajiwa kuzikwa
keshokutwa Jumanne katika Makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam,
huku mazishi yake yakitanguliwa na shughuli ya kumuaga katika Viwanja
vya Leaders Club, saa 2 kamili asubuhi.
Akizungumza
leo mchana, jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Maafa na Sherehe wa
Chama Cha Waigizaji mkoani Dar es Salaam, Kaftany Masoud, alisema
taratibu za mazishi yake zitaanza kwa kuagwa Leaders Club.
Katika
hatua nyingine, msanii wa maigizo na filamu, anayejulikana kwa jina la
Ridhiwan Masoud, amefariki leo mchana katika Hospitali ya Taifa,
Muhimbili, hivyo kuendeleza wimbi la misiba ya wasanii na wanamuziki
Tanzania, ukiwamo msiba wa Amina Ngaluma, mwanamuziki wa dansi, ambaye
jumanne na Jumatano mwili wake utaletwa Tanzania tayari kwa masishi
yake.
Msiba wa msanii huyo upo maeneo ya Magomeni Mapipa, mtaa wa Mkadini, ambapo ndipo zitakavyoendelea taratibu za mazishi yake.
No comments:
Post a Comment