Baada
ya Moyes kumalizana na Man United na kuvunja mkataba, hakuna ubishi
ilikuwa ni lazima aondoke na kwenda kupumzika nje ya England.
Moyes alichagua Marekani, aliona ingekuwa sehemu nzuri ambayo angeweza kujipumzisha kabla ya kuanza upya maisha ya mapambano.
Kwa
kuwa aliamua kwenda katika Mji wa Florida akiwa na mkewe na baada ya
kulijua hilo, bilionea Glazer alimpa Moyes ofa nyingine ya kufikia
katika nyumba yake ya kifahari iliyo mjini humo.
Pia atapata huduma ya usafiri na usimamizi wa kutembezwa sehemu mbalimbali za jiji hilo na wasaidizi wa Glazer.
Utaona
hivi, kocha akivunja mkataba au klabu kufanya hivyo. Basi uadui
unatangulia na ikiwezekana viongozi wa klabu hawataki hata kuzungumza na
kocha kwa kuwa anaonekana kama ni adui.
Glazer
ndiye anayepitisha uamuzi wa mwisho, lakini anaonyesha kiasi gani
walivyoachana kistaarabu na Moyes na hakuna tatizo lolote lililotokea.
Hivyo mambo yako kitaalamu zaidi ndiyo maana wakati mashabiki wanaendelea kupiga kelele. Moyes anakula ‘bata’ Marekani.
Fin.
Moyes
amelipwa fedha hizo ambazo zinajumuisha mshahara wake wa mwezi, fedha
ya kuvunja mkataba pamoja na malipo ya usumbufu kutokana na uvunjani huo
wa mkataba.
Lakini
wakati wa uvunjani mkataba wake, kuna mambo kadhaa ya kiufundi
yalifanyika ambayo yanaashiria namna gani walioendelea katika michezo,
mikataba yao inavyokuwa na utaalamu.
Katika
mkataba wa Moyes, ilikuwa hivi. Kama angeifikisha timu katika nne bora
na kuweza kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya, basi wakimfukuza ilikuwa ni
lazima alipwe kitita cha pauni milioni 9 (zaidi ya Sh bilioni 22.5).
Pamoja
na maji kuwafika shingoni, uongozi wa Man United uliendelea kufanya
subira katika jambo moja. Kuwa iwapo watafungwa mechi itakayothibitisha
kuwa hawatakuwa katika nne, maana yake wamekosa kushiriki Ligi ya
Mabingwa Ulaya, hapo watatoa pauni milioni 7 badala ya milioni 9.
Mkutano
wa mwisho waliofanya wamiliki wa Man United, Joe Glazer na wenzake
ilikuwa ni kujaribu kuokoa pauni hizo milioni 2 wakati Moyes anaondoka.
Mechi
dhidi ya Everton ndiyo ilikuwa na majibu, kama Man United wangepoteza
maana yake uhakika wasingefika nne bora na malengo ya uongozi kuokoa
pauni milioni 2 ungekuwa umetimia.
Baada
ya Man United kufungwa mabao 2-0, viongozi wa Man United waliandaa
mkutano mara moja kumtaarifu kocha huyo kuhusiana na suala hilo na
taarifa zikaanza kuvuja.
Huenda
wengi walishangazwa na namna ungozi wa Man United ulivyochelewa
kumuondoa. Lakini mambo mawili yalikuwa ya msingi zaidi kwao kuliko
matakwa ya mashabiki.
Kwanza
kuangalia kama kungekuwa na mabadiliko ili Moyes aendelee, lakini
kuhakikisha kama imeshindikana, basi na pauni milioni 2 ambazo si haba,
ziokolewe.
Hilo
ni moja la kujifunza kwa klabu za hapa nyumbani namna ambavyo mikataba
inaandaliwa kitaalamu na inakuwa imelenga mambo kadhaa na hata
ukivunjika. Zaidi unalenda kwenye kufanikiwa na kufeli na si ilimradi
mkataba tu wa kazi, hata wa kocha unaringana na wafanyakazi wote!
Kitu cha pili cha kujifunza ni
No comments:
Post a Comment