Kwenye
mechi kati ya Barcelona na Villareal kuna shabiki mmoja alimrushia
ndizi Mbrazil Dani Alves anaeichezea Barca kitendo ambacho kilionyesha
kabisa ni ubaguzi wa kufananishwa na Nyani ambapo Dani aliiokota ndizi
hiyo na kuila kabla ya kupiga mpira wa kona na kuifanya kama sio ishu.
Baada
ya hapo Dani alisema aliamua kula ndizi hiyo kwa sababu baba yake mzazi
aliwahi kumwambia kuhusu umuhimu wa mwili wa mwanadamu kupata ndizi.
Ni
kitendo kilichosifiwa sana na baadae kuwa topic kubwa ambapo mastaa
mbalimbali wamejitokeza kumsupport Dani na kupinga ubaguzi kwa kupiga
picha wakiwa wanakula ndizi ambapo miongoni mwao ni Staa wa muziki
kutoka Nigeria Davido, mastaa wa soka kama Emmanuel Adebayor, Samuel
Eto’o, Neymar na wengine kama wanavyoonekana hapa chini.
No comments:
Post a Comment