KLABU
ya Villarreal imempiga marufuku ya kudumu ya kutoingia katika uwanja
wake wa El Madrigal shabiki aliyemrushia ndizi beki wa kulia wa FC
Barcelona, Dani Alves kwenye mchezo wa La Liga jana jumapili.
Beki
huyo wa kibrazil baada ya kurushiwa ndizi hiyo aliiokota na kuila
wakati akiwa katika harakati za kupiga kona, na kitendo hicho kilionesha
shukurani za kejeli kwa shabiki aliyefanya jambo hilo la kibaguzi.
Katika mechi hiyo Barca walitoka nyuma kwa mabao 2-0 na kushinda 3-2.
Villarreal
wamethibitisha kumpa kifungo cha kidumu shabiki huyo na kusitisha
tiketi zake za msimu huu, huku wakitarajia kumchukulia hatua kali zaidi
juu ya ishara ya ubaguzi wa rangi aliyoionesha jana.
“Villarreal
inaitangazia dunia kuwa imekerwa sana na kuchukizwa na kitendo
kilichotokea jana kwenye mechi dhidi ya FC Barcelona ambapo shabiki
alirusha ndizi katika uwanja El Madrigal”. Taarifa ya klabu imesomeka.
“Shukurani
kwa maafisa usalama na mashabiki wote. Klabu imefanikiwa kumbaini
shabiki huyo na kuamua kufuta tiketi zake za msimu huu na kumfungia
kifungo cha kudumu kutoingia katika uwanja wa El Madrigal”
“Kwa
mara nyingine tena, klabu inapenda kueleza msimamo wake juu ya heshima,
usawa, undugu na mchezo wa kiungwana ndani na nje ya uwanja na
haitavumilia uvunjifu wa kanuni hizi kama vile kuleta fujo na ubaguzi wa
rangi”.
Kitendo
alichofanyiwa Alves jana kimemkera Mbrazil mwenzake aliyeweka picha
katika mitandao ya kijamii akila ndizi kama ishara ya kumuunga mkono
kaka yake huyo mweye miaka 30 na kuandika maneno chini ya picha
yaliyosema: “Sisi wote ni nyani”.
Mabao
mawili ya kujifunga na lile la Lionel Messi yaliwafanya Barca kwa mbali
waanze kufufua matumaini ya kutwaa ubingwa katika wiki hii ngumu ambayo
wamempoteza kocha wao wa zamani, Tito Vilanova
No comments:
Post a Comment