Kwa mujibu wa ripota wa nguvu kwenye maelezo ambayo hayajathibitishwa na mamlaka husika, ndege hii ya shirika la ndege la Kenya ilitoka nje ya njia kidogo kwa tairi zake za
nyuma kuingia kwenye majani.
Chanzo kinatajwa kuwa ukungu uliokua umezidi kutokana na mvua zinazonyesha Dar es salaam sasa hivi hivyo kumpa rubani yeyote tabu ya kuona vizuri ambapo kuanzia tukio lilipotokea mida ya saa nane mchana, ndege kubwa hazikuruhusiwa kutua wala kupaa kutokana na ukungu lakini pia kutokana na ndege hii iliyokua imesimama sehemu isiyotakiwa.
Hakuna mtu yeyote alieumia kwa sababu ndege ilitua salama ambapo sasa hivi wameshaitoa na kuipeleka kwenye sehemu ya kutengenezea ndege.
Naambiwa ni ndege ndogo za Zanzibar peke yake zilizokua zinaruhusiwa kutua.
No comments:
Post a Comment